Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Hatma ya Uingereza kujulikana baada ya uchaguzi

media Mmoja wa waandamanaji wanaopinga Uingerza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya akishikilia bendera ya Umoja wa Ulaya mbele ya makao makuu ya Bunge hukoLondon, Uingereza, Oktoba 25, 2019. REUTERS/Henry Nicholls

Wananchi wa Uingereza hivi leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa tatu kufanyika chini ya miaka mitano, uchaguzi ambao unatajwa kuwa ndio utakaotoa hatma ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Uchaguzi huu unafuatia ule wa mwaka 2015 na 2017, ambapo uchaguzi wa safari hii unatajwa kuwa wa ushindani ukilinganisha na ule uliyopita, kutokana na hofu kuwa vyama vidogo huenda vikafanya maajabu.

Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura umetabiri kwamba matokeo ya uchaguzi yatakaribiana katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wenye lengo la kutatua mzozo wa Brexit.

Bunge la Uingereza mara kadhaa lilikataa kukubali masharti ya kuachana na Umoja wa Ulaya ambapo waziri mkuu wa zamani theresa May alikubaliana na Umoja huo, na kumlazimisha kuacha madaraka na kumuingiza Johnson katika mzozo huo akiahidi kuupatia ufumbuzi. Boris Johnson aliahidi kuiondoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya ifikapo Januari 31.

Mchuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya waziri mkuu Boris Johnson na mpinzani wake Jeremy Corbyn ambao kila mmoja amejinasibu kukamilisha mchakato wa Brexit.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana