Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UCHAGUZI-SIASA-BORIS-JEREMY

Kampeni zaingia katika kipindi cha lala salama nchini Uingereza

Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Uingereza unaotarajiwa kufanyika Alhamisi ya wiki hii zimeingia hatua ya lala salama huku waziri mkuu Boris Johnson na mpinzani wake Jeremy Corbyn wakijaribu kuwashawishi wananchi kuwaunga mkono.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiendelea na kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu 12.12.2019
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiendelea na kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu 12.12.2019 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika uchaguzi huu Waziri Mkuu Johnson atajaribu kurejesha wingi wa viti bungeni baada ya mtangulizi wake Theresa May kupoteza katika uchaguzi wa miaka 2 iliyopita, huku kiongozi wa chama cha Labour, Jeremy Corbyn kwa upande wake akiwa na imani ya kuongeza wabunge zaidi.

Ajenda kubwa katika uchaguzi huu ni suala la nchi hiyo kujitoa kwenye umoja wa Ulaya, ambapo huenda kukawa na sintofahamu zaidi ikiwa Boris Johnson atashindwa kupata ushindi wa jumla.

Hapo jana waziri mkuu Johnson amesema matokeo ya uchaguzi wa Alhamisi yataishi kwa miongo kadhaa katika siasa za nchi hiyo, huku akiahidi kutekeleza mchakato wa Brexit ikiwa atashinda.

Ijumaa ya wiki iliyopita, Boris Johnson na Jeremy Corbyn walifanya mdahalo wao wa mwisho wa televisheni, ambapo kila mmoja alimtuhumu mwingine kwa kushindwa kuweka mbele maslahi ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.