Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAANDAMANO-UCHUMI

Mgomo dhidi ya Mageuzi ya hazina ya uzeeni waendelea Ufaransa

Usafiri wa umma, umeendelea kwa siku ya pili leo Ijumaa nchini Ufaransa, baada ya kuanza kwa mgomo wa wafanyakazi katika sekta mbalimbali nchini humo.

Matukio ya kwanza jijini Paris wakati wa maandamano dhidi ya mageuzi ya pensheni, Desemba 5, 2019.
Matukio ya kwanza jijini Paris wakati wa maandamano dhidi ya mageuzi ya pensheni, Desemba 5, 2019. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi katika sekta mbali mbali nchini humo wamegoma na wanaandamana, kupinga mageuzi kuhusu mfumo wa pensheni nchini humo.

Siku ya Alhamisi, watu zaidi ya 800,000 waliandamana katika barabara za miji mbalimbali nchini humo, huku machafuko yakiripotiwa katika maeneo ya miji.

Mgomo huu umeathiri safari za ndani katika usafiri wa ndege, huku sehemu chache za jiji kuu Paris, zikitarajiwa kushuhudia hali kuwa kama kawaida.

Viongozi wa wafanyakazi watakutana leo Ijumaa, kuamua iwapo mgomo na maandamano vitaendelea katika siku zijazo,

Wafanyakazi nchini Ufaransa wanasema hawataki mabadiliko hayo ambayo wanasema yataathiri masiha yao, kuelekea na baada ya kustaafu na namna watakavyopata mafao yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.