Pata taarifa kuu
UJERUMANI-URUSI-USHIRIKIANO

Mauaji ya raia mmoja wa Georgia Berlin: Ujerumani yawafukuza wanadiplomasia wawili wa Urusi

Ujerumani imechukuwa uamuzi wa kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Urusi kwa sababu ya mamlaka ya Moscow kukataa kushirikiana katika uchunguzi wa mauaji ya raia mmoja kutoka Georgia mwezi Agosti mwaka huu jijini Berlin.

Mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.
Mji mkuu wa Ujerumani, Berlin. RFI/Pascal Thibaut
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, ambayo imenukuliwa na mashirika ya Habari ya Urusi, imeahidi kujibu hatua hiyo 'isio kuwa ya kirafiki' na 'isio kuwa na haki'.

Zelimkhan Khangoshvili, mwenye umri wa miaka 40, mpiganaji wa zamani aliyekuwa akiinga mkono kujitawala kwa Chechnya, raia wa Georgia, alipigwa risasi mara mbili kichwani kwenye mbuga ya katikati ya mji mkuu wa Ujerumani akielekea msikitini.

Ofisi ya Mashtaka ya Ujerumani imeweka kesi hiyo mikononi mwake na imesema ina uhakika kwamba mauaji hayo yaliagizwa na Urusi au Jamhuri ya Urusi ya Chechnya.

Kremlin imeendelea kukanusha kuhusika kwa njia yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.