Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Usalama: Viongozi wa NATO wakutana kwa mazungumzo London

media Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) wanatarajia kujelezea kwenye mkutano wa kilele wa NATO (picha ya kumbukumbu). LUDOVIC MARIN / POOL / AFP

Viongozi kutoka nchi zinazounda Umoja wa jeshi la kujihami kwa nchi za Magharibi NATO, wanakutana jijini London kujadili masuala mbalimbali ya usalama na ushirikiano kati yao.

Mkutano huu unafanyika nchini Uingereza, siku kumi kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Tayari Rais wa Marekani Donald Trump amewasili jijini London, na kuelekea katika mkutano huu amekuwa akijigamba kuwa, tangu aingie madarakani, nchi wanachama wa NATO zimeimarisha uwajibikaji wao, kinyume na ilivyokuwa zamani.

Kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo wa sabini wa NATO, Rais Trump na viongozi wengine wa dunia, watakuwa na dhifa na Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili.

Mbali na mkutano huo wa NATO, viongozi wengine wa dunia kama vile Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wanatarajiwa kukutana pembezoni mwa mkutano huo kujadili ushirikiano kati ya nchi zao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana