Pata taarifa kuu
UFARANSA-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Emmanuel Macron atangaza makubaliano kati ya China na EU kuhusu PGI

Kando na ziara yake nchini China, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kwamba Umoja wa Ulaya na China zitatia saini Jumatano hii Novemba 6 mjini Beijing mkataba uliosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu masuala ya kijiografia (PGI).

Rais Macron alianza ziara yake ya pili ya kiserikali nchini China Novemba 4, 2019 katika kituo cha kifedha cha Shanghai, ambapo amehudhiria maonyesho ya bidhaa za kuagizwa kutoka nchi za nje, Shangai.
Rais Macron alianza ziara yake ya pili ya kiserikali nchini China Novemba 4, 2019 katika kituo cha kifedha cha Shanghai, ambapo amehudhiria maonyesho ya bidhaa za kuagizwa kutoka nchi za nje, Shangai. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo utawezesha kulinda katika mazingira mazuri mazao ya kilimo ya Ulaya yanayoingia katika soko la China.

"Mkataba huo kuhusu PGI uliosubiriwa kwa muda mrefu," utakuwa na "maendeleo muhimu sana, ambayo ni matokeo ya hatua za pamoja" katika ngazi ya Ulaya, amesema rais wa Ufaransa siku ya kwanza ya ziara yake nchini China.

Mkataba huu "utawezesha kukuza na kubadilishana biashara kwa kulinda chapa zetu, hakimiliki za ujuzi," ameongeza Emmanuel Macron. Kwa upande wa rais wa Ufaransa, amesema "tunajua jinsi ya kujenga, kwa ustadi wa hali ya juu, ajenda chanya ya biashara".

Mkataba huo utasainiwa kando na mazungumzo ya Jumatano wiki hii jijini Beijing kati ya Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, huku kukiwa na mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani.

Mkataba huo unahusu bidhaa 100 kutoka Ulaya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anazuru China wakati kuna shinikizo la kuitaka China kufungua masoko yake, licha ya mizozo iliyopo ya kibiashara.

Macron aliwasili Shangai Jumanne wiki hii na kutembelea maonyesho ya bidhaa za kuagizwa kutoka nchi za nje.

Ziara hiyo imejiri wakati Ufaransa na washirika wake wanaitaka China kutekeleza ahadi zake za kuongeza bidhaa za kilimo na za kiviwanda inazonunua kutoka nchi za nje, na pia itanue masoko yake ya kifedha na ya huduma nyinginezo.

Ufaransa na Umoja wa Ulaya zimeungana na Marekani kulalamika dhidi ya biashara za China zikisema zimekosa usawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.