Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Hatma ya Uingereza kujulikana Ijumaa hii

Mabalozi kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya wanakutana leo, kujadili hatima ya Uingerereza katika Umoja huo na kuamua nchi hiyo iongezewe muda gani, ili wabunge wapitishe mapendekezo mapya ya kujiondoa kwenye umoja huo.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Uingereza alitangaza kwamba nchi yake na Uingereza zilifikia mkataba mpya mzuri wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Uingereza alitangaza kwamba nchi yake na Uingereza zilifikia mkataba mpya mzuri wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, baadhi ya mabalozi hao, wanataka Uingereza ipewe muda wa miezi mitatu.

Tayari Waziri Mkuu Boris Johnson amesema kuwa, iwapo wataongezewa muda hadi mwezi Januari mwaka 2020, ataitisha Uchaguzi Mkuu wa mapema.

Johnson bado anaendelea kusisitiza kuwa anataka Uingereza iondoke kwenye Umoja huo ifikapo tarehe 31 mwezi huu.

Johnson amesema uchaguzi unaweza ukahitajika kama kuondoa mkwamo wa Brexit, lakini chama cha upinzani cha Labour kimetaka kujadiliwa kwanza kwa tarehe ya mwisho ya Brexit ambayo ni Oktoba 31.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.