Mkataba mpya wa Brexit wafikiwa kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya
Mkataba mpya wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya umefikiwa Alhamisi wiki hii, Oktoba 17, kabla ya mkutano muhimu wa Umoja wa Ulaya.
Imechapishwa:
Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker ametangaza kwenye Twitter kuwa mkataba umefikiwa mjini Brussels. Boris Johnson pia ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akikaribisha "mkataba mpya mzuri".
Mkataba huu ambao umefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu ambayo yametajwa na Jean-Claude Juncker kama "ya haki na usawa" yanaweza kuanza kutumika Novemba 1, 2019.
Nakala hii sasa itawasilishwa kwa Wakuu wa Nchi na Serikali ambao walikuwa wanatarajiwa kufanya kikao chao cha kwanza cha kazi jijini Brussels baadaye leo alaasiri.
Viongozi hao wanatarajia kutoa idhni yao kwa mapendekezo ya Michel Barnier, ambaye amesema watu wasisubiri maajabu, kwa hatua hii.