Pata taarifa kuu
UFARANSA-CHIRAC-KIFO-ULAYA

Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac afariki dunia

Raia wa Ufaransa wanaomboleza kifo cha aliyekuwa rais wao Jacques Chirac, atakayekumbukwa kwa jitihada zake za kuiongoza nchi yake kuhamasisha Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac aliyefariki dunia Septemba 26 2019
Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac aliyefariki dunia Septemba 26 2019 AFP Photos/POOL/Patrick Kovarik
Matangazo ya kibiashara

Chirac amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86, na aliongoza nchi hiyo kwa mihula miwili kati ya mwaka 1995-2007.

Aidha, aliwahi kuhudumu kama Waziri Mkuu kati ya mwaka 1974-1976 na baadaye kati ya mwaka 1986 hadi 1988.

Familia yake imesema , rais huyo wa zamani alifariki dunia akiwa amezingirwa na familia yake Alhamisi asubuhi.

Marais wa zamani wa Nicolas Sarkozy na François Hollande wamesema Ufaransa imempoteza kiongozi shupavu aliyesimamia kwa uaminifu tunu za nchi hiyo.

Wabunge walitumia muda wa dakika moja katika vikao vyao kumkumbuka rais huyo wa zamani ambaye wamemwelezea kama kiongozi aliyechangia pakubwa maendelep ya Umoja wa Ulaya, licha ya kukumbwa na kashfa za ufisadi wakati akimalizia uongozi wake.

Jean-Claude Juncker, rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya na rais wa zamani wa Luxembourg, amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kuaga dunia kwa Chirac na kusema Ulaya imempoteza mtu muhimu na binafsi amempoteza rafiki wa karibu.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel naye amesema, amesikitishwa na kifo cha Chirac na kumwelezea kama mshirika wa karibu na rafiki.

Rais Emmanuel Macron anatarajiwa kulihotubia taifa baadaye Alhamisi usiku kuhusu kifo cha mtangulizi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.