Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Brexit: Waziri Mkuu wa Uingereza apata pigo jingine jipya kuhusu uchaguzi wa mapema

Shughuli za Bunge la Uingereza zimesitishwa mapema Jumanne asubuhi kwa muda wa wiki tano, hadi Oktoba 14, sawa na wiki mbili tu kabla ya tarehe iliyopangwa ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya (Brexit).

Makao makuu ya Bunge la Uingereza, London Septemba 4, 2019.
Makao makuu ya Bunge la Uingereza, London Septemba 4, 2019. © REUTERS/Hannah McKay
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja baada ya wabunge kukataa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema uliotakiwa na Waziri Mkuu kutoka chama cha Conservative Boris Johnson.

Wabunge wa Uingereza wamemkatalia katu katu kwa mara nyingine Waziri Mkuu Boris Johnson kufanyika kwa uchaguziwa wa mapema, kabla ya shughuli za Bunge kusimamishwa hadi Oktoba 14, wiki mbili tu kabla ya tarehe iliyopangwa ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya (Brexit).

Waziri Mkuu Boris Johnson ameambulia patupu baada ya kuangushwa kwa kura 293, na hivyo uamuzi wake wa kuitisha uchaguzi wa mapema kwenfa kombo. Pendekezo lake lilihitaji theluthi mbili ya viti vinavyohitajika ili kuistishwa uchaguzi wa mapema.

Boris Johnson alikuwa ametaka uchaguzi wa mapem ufanyike Oktoba 15.

Kabla ya kura kupigwa, Boris JOhnson alihakikishia kwamba hataomba "kuahirishwa tena" kwa mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya (Brexit), zoezi ambalo lilipangwa kufanyika Oktoba 31, licha ya sheria ambayo ilianza kutumika Jumatatu baada ya idhini ya Malkia Elizabeth II.

Kufikisha malalamiko yake mahakamani, kujiuzulu au kuchukua hatua nyingine, Boris Johnson hajaelezea jinsi atashughulikia suala hilo.

"Ikiwa mnataka tarehe ya mwisho, basi pigeni kura kwa Uchaguzi Mkuu!", Boris Johnson amemwambia kiongozi wa upinzaji Jeremy Corbyn ambaye amesema anaogopa kushindwa kwenye uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.