Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-KANISA-HAKI

Udhalilishaji wa kingono dhidi ya watoto: Rufaa ya Kadinali George Pell yakataliwa

Mahakama nchini Australia imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na aliyekuwa kiongozi wa juu wa kanisa katoliki Kadinali George Pell, ambaye alihukumiwa kwa makosa ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya watoto.

Kardinali George Pell akiondoka mahakamani huko Melbourne, Mei 1, 2018
Kardinali George Pell akiondoka mahakamani huko Melbourne, Mei 1, 2018 AFP
Matangazo ya kibiashara

Pell ambaye alihusika na masuala ya fedha na kuwa miongoni mwa watu wa karibu wa kiongozi wa kanisa hilo Papa Francis, sasa atendelea kutumikia kifungo chake cha miaka 6 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuwadhalilisha kingono watoto wawili wa miaka 13 katika miaka ya 1990.

Pell ambaye kwa mujibu wa sheria za Australia huenda akafikiriwa kuachiwa huru baada ya miaka mitatu na miezi 8, bado anaweza kwenda katika mahakama ya juu kutaka isikilize tena rufaa yake.

Mawakili wanaomtetea Pell wamepinga karibu hoja 13 za upande wa mashtaka, kuanzia kwenye uhalali wa baadhi ya mashahidi, akiwemo shahidi mkuu na kuonesha mashaka kuhusu ushahidi uliowasilishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.