Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 07/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Waziri mkuu mpya wa Uingereza kutangazwa Jumanne hii

media Boris Johnson na Jeremy Hunt, wagombea ambao mmoja wao anatarajia kumrithi Theresa May kama waziri mkuu mpya wa Uingereza, wakati wa mjadala wa televisheni, Manchester Julai 9, 2019. Matt Frost / ITV / AFP

Mwanasiasa wa Uingereza na Meya wa zamani wa London, Boris Johnson Jumanne wiki hii anatarajiwa kutangazwa kuwa waziri mkuu mpya ambaye atakuwa na jukumu la kuhakikisha nchi hiyo inajitoa kwenye Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31.

Johnson ambaye katika kampeni zake ameapa kuhakikisha nchi hiyo inatoka ikiwa na mkataba au bila ya mkataba, anatarajiwa kukumbana na changamoto kubwa katika utekelezaji wa azma yake ikiwemo suala la Iran.

Licha ya kuwa Boris Johson anatarajiwa kushinda kiurahisi nafasi hiyo, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Jeremy Hunt, ambaye licha ya kutoonekana kupewa nafasi, lakini ana uungwaji mkono wa wabunge wengi.

Suala la uamuzi wa nani atakuwa waziri mkuu ajae wa Uingereza sasa limebaki mikononi mwa Tory ambao leo wataamua ikiwa watamkabidhi kijiti Boris Johnson au kubadili karata zao na kumkabidhi kijiti Jeremy Hunt kuchukua nafasi ya Theresa May aliyejiuzulu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana