Pata taarifa kuu
UJERUMANI-EU-UCHUMI-SIASA

Ursula von der Leyen achaguliwa mkuu wa Tume ya Ulaya

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ,Ursula von der Leyen, amechaguliwa Mkuu wa Tume ya Ulaya. Bunge la Ulaya limethibitisha uteuzi wake na hivo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taasisi kuu ya Umoja wa Ulaya.

Rais mteule wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, akitoa hotuba wakati wa mjadala kuhusu uchaguzi wake kwa Bunge la Ulaya, Strasbourg tarehe 16 Julai 2019.
Rais mteule wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, akitoa hotuba wakati wa mjadala kuhusu uchaguzi wake kwa Bunge la Ulaya, Strasbourg tarehe 16 Julai 2019. REUTERS / Vincent Kessler
Matangazo ya kibiashara

Uthibitishwaji huo ulihitaji wingi wa kura 374 na waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani anaendoka alipita kwa ziada ya kura tisa.

Mtangulizi wake, Jean-Claude Juncker ambaye ni kutoka chama cha EPP, alipata kura 422 zaidi ya 376 zilizohitajika mnamo mwezi Julai 2014.

Ursula von Leyen ambaye anahudumu mpaka sasa katika serikali ya Angela Merkel kama Waziri wa Ulinzi, alizaliwa jijini Brussels miaka sitini iliyopita wakati baba yake, Ernst Albrecht, alikuwa akifanya kazi katika Tume ya Ulaya. Anakuwa mwanamke wa kwanza kuchukua nafasi hiyo.

Von der Leyen aliwamabia wabunge mjini Strasbourg Jumanne kuwa suala la jinsia litakuwa sehemu muhimu ya kazi yake.

Aliibuka kama mgombea wa mwisho na wabunge wengi walikuwa na hasira kwa sababu hakuna kati ya mgombea wao alichaguliwa kwa wadhifa huo. "Ujumbe wangu kwenu nyote: Tushirikiane kwa kujenga," alisema.

Von der Leyen ameainisha ajenda yake ya kisiasa kwenye Ulaya ya kijani zaidi na yenye usawa wa kijinsia ambako utawala wa sheria unaendelea kuheshimiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.