Pata taarifa kuu
UINGEREZA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Vita vya maneno vyaibuka kati ya Uingereza na Marekani

Marekani na Uingereza vimeendelea kurushiana maneno kufuatia mvutano wa kidiplomasia unaoendelea kati ya nchi hizi mbili kwa siku tatu sasa, hali ambayo inaendelea kuzua sintofahamu.

Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May wakiongea wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na mkewe Trump, Melania Trump, Winfield House wakati wa ziara yao rasmi London Juni 4, 2019.
Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May wakiongea wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na mkewe Trump, Melania Trump, Winfield House wakati wa ziara yao rasmi London Juni 4, 2019. Chris Jackson / Poool via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kumshambulia na kumuita mjinga Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na balozi wake mjini Washington, Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt amekuja juu na kuesema, “Donald Trump amemkosea heshima waziri mkuu wa Uingereza”.

Kulingana na barua zilizovuja balozi wa uingereza nchini Marekani Kim Darrach aliueleza utawala wa Donald Trump kama usiofaa.

Sir Kim anawakilisha malkia wa Uingereza na serikali ya Uingereza nchini Marekani.

Katika barua pepe zilizofichuliwa siku ya Jumapili, Sir Kim aliutajaa utawala wa rais Trump kama usiofanya kazi na usiojielewa. Wakati huo huo Bi May alisema kuwa ana imani na Sir kim lakini hakubaliana naye kwa maneno hayo.

Baada ya kukasirishwa na hatua ya Theresa May kumuunga mkono balozi huyo, Rais trump alimshtumu Bi May na kuanza kusema vile alivyoshindwa kusimamia Brexit.

Mvutano huu unaendelea kuzua sntofahamu kati ya nchi hizi mblili. Mkutano kati ya waziri wa maswala ya biashara za kimataifa nchini Uingereza Liam Fox na waziri wa biashara wa Marekani Wilbur Ross ulifutiliwa mbali siku ya Jumanne.

Mapema siku ya Jumanne Bwana Trump alituma ujumbe wa twitter akisema: Balozi wa Uingereza ambaye ameletwa hapa Marekani sio mtu tunayemshabikia , ni mtu 'mjinga sana'.

Awali serikali ya Uingereza ilitaja ufichuzi huo kama bahati mbaya na imeanza uchunguzi ramsi. Huku ikisema kuwa Uingereza na Marekani bado zina uhusiano maalum na wa kudumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.