Pata taarifa kuu
MAREKANI-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Balozi wa Uingereza nchini Marekani aachia ngazi

Balozi wa Uingereza nchini Marekani, Kim Darroch, ametangaza kujiuzulu Jumatano wiki hii baada ya kuingia utata na rais wa Marekani kufuatia kuibuka kwa mvutano wa kidiplomasia kutokana na kuvuja kwa barua pepe za siri kutoka kwa balozi huyo.

Balozi wa Uingereza nchini Marekani Kim Darroch ambaye ametangaza kujiuzulu Jumatano, Julai 10, 2019.
Balozi wa Uingereza nchini Marekani Kim Darroch ambaye ametangaza kujiuzulu Jumatano, Julai 10, 2019. © Paul Morigi / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tangu kuvuja kwa nyaraka rasmi kutoka kwa ubalozi huu, kumekuwa na maoni tofauti kuhusu nafasi ninayoshikilia na muhul wangu kama balozi. Nataka kukomesha hali hii. hali inayojiri kwa sasa hainiruhusu kuendelea na majukumu yangu kama inavyotakiwa, "balozi Darroch ameelezea katika barua aliomuandikia Simon McDonald, mkuu wa idara inayohusika na masuala ya kidiplomasia ya Uingereza.

Baada ya kuvuja kwa barua hizoi, Donald Trump ameendelea kuhakikisha kwamba hatakuwa na "mawasiliano" na Kim Darroch.

"Kwa hali hii inayojiri, njia inayobaki pekeeni kuteua balozi mpya," balozi Darroch ameandika.

Waziri Mkuu anaye maliza muda wake Theresa May, ambaye alishambuliwa kwa maneno na Donald Trump baada ya kumuunga mkono Kim Darroch, amesikitika kuhusu uamuzi wa mwanadiplomasia huyo.

"Ni masikitiko makubwa kuona anachukua uamuzi kama huo wa kujiuzulu kwenye nafasi yake," Theresa May amesema Jumatano wiki hii wakati wa maswali ya kila wiki ya bunge.

"Serikali nzuri inategemea uwezo wa maofisa wa kutoa ushauri kamili na wa wazi, na nataka maofisa wetu wote wawe na ujasiri wa kufanya hivyo," Bi May amesema.

"Mimi pia ninasikitishwa na uamuzi wa kujiuzulu wa Kim Darroch," amesema Jeremy Corbyn, kiongozi wa upinzani kutoka chama cha Labour, akitoa wito kwa Bunge kumuunga mkono balozi Darroch.

Barua pepe za siri kutoka kwa balozi huyo wa Uingereza zilikuwa na msururu wa ukosoaji wa utawala wa rais Trump na kusema kuwa Ikulu ya Whitehouse ilikuwa haina utendakazi wa haja na kwamba kulikuwa na mgawanyiko mkubwa chini ya uongozi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.