Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Mtuhumiwa wa shambulio la msikiti New Zealand akana mashtaka dhidi yake

media Brenton Tarrant, mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya waumini 51 wa kiislamu kwenye mji wa Christchurch. Mark Mitchell/New Zealand Herald/Pool via REUTERS

Mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya watu 51 aliowapiga risasi wakiwa msikitini kwenye mji wa Christchurch nchini New Zealand mwezi machi mwaka huu, amekana mashtaka yote yanayomkabili.

Mwanasheria wa Brenton Tarrant mwenye umri wa miaka 28, amesema mteja wake amekana mashtaka yote 51 ya mauaji, 40 ya jaribio la kuua na moja la kutekeleza kitendo cha kigaidi.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashtaka ya ugaidi kusikilizwa kwenye mahakama za New Zealand.

Tarrant mwenyewe hakuwepo mahakamani wakati kesi yake ikisikilizwa lakini alionekana kupitia picha za video kutoka kwenye jela ambako anashikiliwa.

Katika muda wote wa karibu dakika 30, Tarrant hakusema kitu chochote mbali ya wakati mmoja kutikisa kichwa chake kuonesha ishara kuwa alikuwa anamsikia jaji anayesikiliza kesi yake.

Wakati mwanasheria wake amesimama na kusema kuwa mteja wake anakana mashtaka dhidi yake, Tarrant alionekana kuonesha ishara ya kukonyeza kwenye kamera iliyokuwa ikirekodi.

Tarrant ambaye amjipambanua kama mzungu mwenye msimamo mkali, anatuhumiwa kuhusika peke yake katika tukio la Machi 15, ambapo akiwa na bunduki aliingia msikitini na kuanza kuwafyatulia risasi waumini.

Serikali ya New Zealand tayari imepitisha sheria kali dhidi ya wamiliki wa aina ya silaha ambayo ilitumiwa na Tarrant.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana