Pata taarifa kuu
TRUMP-MAREKANI-UINGEREZA-ZIARA-DIPLOMASIA

Rais wa Marekani Donald Trump azuru Uingereza

Rais wa Marekani Donald Trump ameanza  ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Ungereza, ziara ambayo anaifanya wakati huu taifa hilo likijaribu kupata makubaliano na umoja wa Ulaya kuhusu mpango wake wa kujitoa.

Rais wa Marekani  Donald Trump na mkewe  Melania Trump wakisafiri kwenda Uingereza Juni 2 2019
Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump wakisafiri kwenda Uingereza Juni 2 2019 (REUTERS/Carlos Barria)
Matangazo ya kibiashara

Ni ziara ambayo imekuwa gumzo kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya rais Trump ambaye alisema wazi kuwa anamuunga mkono kiongozi wa upinzani Nigel Farage na kwamba angepaswa kujumuishwa kwenye mazungumzo ya nchi hiyo kujitoa.

Tayari wanaharakati wamepanga kufanya maandamano makubwa jijini London na kwenye miji mingine mikubwa kupinga ziara yake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter wakati akiwasili nchini Uingereza, amemshtumu Meya wa jiji la London, Sadiq Khan kwa kuunga mkono maandamano dhidi yake.

"Meya Khan amefanya kazi mbaya kama Meya wa jiji la London, ameonekana kikwazo kwa ziara ya rais wa Marekani katika nchi ambayo ni mshirika wake wa karibu," aliandika katika ukurasa wake wa Twitter @realDonaldTrump.

Katika mahojiano na gazeti la The Sun, rais Trump mbali na kumuunga mkono farage, pia aliweka wazi kuwa angependelea kuona Boris Johnson anateuliwa kuwa waziri mkuu ajae.

Uingereza inatarajiwa kuwa na Waziri Mkuu mpya hivi karibuni, baada ya Theresa May kutangaza kuwa atajiuzulu tarehe 7 mwezi Juni.

Baada ya kuwasili jijini London, rais Trump ameandalia dhifa maalumu na malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ambapo ataambatana na mke wake Melania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.