Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

New Zealand: Arobaini wauawa katika mashambulizi dhidi ya miskiti miwili Christchurch

media Kikosi maalum cha AOC (Armed Offenders Squad) vinafanya operesheni ya kuwasaka wahalifu walioendesha mashambulizi dhidi ya misikiti miwili huko Christchurch, New Zealand, Machi 15, 2019. REUTERS/SNPA/Martin Hunte

Watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya watu wane kufanya mashambulizi katika msikiti miwili katika mji wa Christchurch, Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema.

Maofisa wa polisi wametumwa katikati mwa jiji la Christchurch baada ya mashambulizi ya risasi katika misikiti miwili nchini New Zealand. Polisi, ambayo inasema "watu wengi wameuawa, imewakamata watu kadhaa.

Kwa mujibu wa chanzo cha polisi katika eneo la tukio, vizuizi vimeanza kuondolewa kwenye barabara za mji huo mara baada ya polisi kutangaza kuwa wamekamata watu wanne na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.

"Watu wane, wanamume watatu na mwanamke mmoja, wanashikiliwa na polisi, " amesema, mkuu wa polisi katika eneo hilo Mike Bush, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, huku akibiani kwamba jeshi lilitegua kilipuzi kilichopatikana katika magari ya watuhumiwa.

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa "gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia".

Awali mkuu wa pilisi katika mji wa Christchurch amesema watu waliouawa ni wengi, lakini hakutaja idadi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana