Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Mpango wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya wafutiliwa mbali

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amepata pigo jingine kubwa baada ya wabunge kufutilia mbali mpango wake wa makubaliano na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu Theresa May akijitetea mbele ya bunge Machi 12, 2019.
Waziri Mkuu Theresa May akijitetea mbele ya bunge Machi 12, 2019. Reuters TV via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo inatokea ikiwa imesalia siku 17 kabla ya kumalizika kwa muda uliyopagwa kuhusu mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Mpango huo umekataliwa kwa kura 391 dhidi ya 242 na kuzua hali ya sintofahamu kwa Uingereza kwa mchakato wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Baada ya kura hiyo ya Jumanne, Waziri Mkuu Theresa May amesema kuwa makubaliano hayo na Umoja wa Ulaya yalikuwa moja ya njia nzuri katika mchakato wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.