Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Kesi ya Benalla: Maseneta washtumu kuzorota kwa shughuli za serikali

media Alexandre Benalla (katikati) akizungukwa na mwenyekiti wa kamati ya bunge la Seneti, Philippe Bas (kushoto) na mwandishi Jean-Pierre Sueur, kwenye makao makuu ya bunge la Senati, Januari 21, 2019. REUTERS/Charles Platiau

Tume ya uchunguzi ya bunge la Seneti nchini Ufaransa kuhusu kesi ya Benalla imesema katika ripoti yake kuwa shughuli nyingi za serikali zilizorota na kuathiri "usalama wa rais" na " maslahi ya taifa".

Baada ya miezi sita ya kazi, watu arobaini wamesikilizwa, na Jumatano ewiki hii kamati ya ya uchguzi ya bunge la Seneti imetoa ripoti yake wakati Alexandre Benalla na Crase wamewekwa chini ya ulinzi tangu Jumanne jioni wakishtumiwa kwamba hawakuheshimu utaratibu wa sheria.

Katika ripoti hiyo, kamati ya bunge la Seneti chini ya uenyekiti wa Philippe Bas (LR), imebaini kile ilichokiita kwamba "mamlaka ya kupita kiasi yaliyopewa mfanyakazi asiyekuwa na ujuzi" katika nyanja ya usalama wa rais, na "ukosefu mkubwa wa tahadhari katika kuzuia migogoro ya kimaslahi kwa baadhi ya wafanyakazi, "ikimaanisha mkataba uliofikiwa na tajiri mkubwa wa Urusi kupitia Alexandre Benalla na Vincent Crase.

Aidha, kamati ya uchunguzi ya bunge la Seneti kuhusu kesi ya Benalla imeomba ofisi ya bunge la Seneti kufungua mashitaka kwa kosa la "ushahidi wa uongo" kutoka wawili hao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana