Serikali ya Malta na Italia zimekataa kuwapokea wahamiaji hao, ambao kwa siku kadhaa sasa wamesalia ndani ya meli hizo.
Papa Francis amewaomba viongozi wa Ulaya kuelewa uhai wa wahamiaji hao na kuwaruhusu kuingia katika mataifa hayo.
Licha ya wito huo ambao pia umetolewa na Tume ya Umoja wa ulaya, serikali ya Malta na Italia zimeonekana kutokuwa tayari kufungua milango yao kwa wahamiaji hao.