Pata taarifa kuu
VATICAN-DINI-IBADA

Krismasi: Papa Francis atoa ujumbe wake wa sita wa Urbi et Orbi

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, amehimiza amani katika nchi za Syria na Yemen, katika ujumbe wake wa Krismasi.

Papa Francis amewataka watu wanaoishi katika nchi zilizoendelea kuishi maisha ya kawaida na kupunguza anasa.
Papa Francis amewataka watu wanaoishi katika nchi zilizoendelea kuishi maisha ya kawaida na kupunguza anasa. REUTERS/Alberto Pizzoli
Matangazo ya kibiashara

Akiongoza misa katika Makao makuu ya Kanisa hilo mjini Vatican, Papa Farncis amesema ana imani kuwa, amani ya kudumu itarejea nchini Syria na Yemen, huku akitoa wito kwa jumuiya ya Kimataifa kuwasaidia watu wanaoteseka hasa watoto.

Aidha, ameshatumu uchoyo miongoni mwa binadamu, suala ambalo amesema limesabisha dunia kukosa upendo.

Viongozi wengi wa dini ya Kikiristo wametumia siku hii kuhubiri amani, haki na mshikamano katika mataifa yao.

Nchini Uganda, Askofu wa wa Kanisa Anglikana, katika eneo la Kusini mwa Ankole Nathan Ahimbi-sibwe katika ujumbe wa krismasi, amemshtumu ufisadi jatikaidara za serikali na mashirika ya kibinfassi , ishara ambayo raia wa nchi hiyo wameanza kuacha njia za Mungu.

Huko nchini Kenya, mbali na wakiristo kufurika Makanisani na wengine katika bustani mbalimbali hasa jijini Naiorbi na fuykwe za Bahari mjini Mombasa, Waziri wa Ulinzi Bi. Rachel Omamo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Samsom Mwathathe, wamewatembela wanajeshi wa Kenya nchini Somalia na kushriki nao chakula cha pamoja.

Nchini Sudan Kusini, raia wa nchi hiyo wamekuwa makanisani kumwomba Mungu kulisaidia taifa hilo kuwa na amani ya kudumu, sawa na mataifa mengine ya Afrika kama Nigeria kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Februari mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.