Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel ajiuzulu

media Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michels, hapa akiwa Brussels tarehe 14 Desemba, amewasilisha barua ya kuiuzulu kwa Mfalme Philippe tarehe 18 Desemba 2018. REUTERS/Piroschka Van De Wouw

Hasira ya wazalendo juu ya mvutano kuhusu uhamiaji umeiangusha serikali ya Ubelgiji na kumlazimu waziri mkuu Charles Michel kutangaza kujiuzulu.

Ikiwa imesalia miezi mitano tu kabla ya kufanyika uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi Mei haikuweza kubainika ikiwa mfalme Philippe angeridhia uamuzi wa ghalfa wa Michel.

Taarifa ya ikulu imesema bado uamuzi unasubiriwa ingawa chanzo kimoja kimesema huenda utawala wa kifalme utaitaka serikali ya Michel kusimamia shughuli za kila siku za serikali hadi pale kalenda ya uchaguzi itakapo tajwa.

Siku ya Jumapili katika mjadala wa bungeni, waziri mkuu huyo, Mliberali alikitri kushindwa kukabiliana na kura ya kutokuwa na imani ambayo iliitishwa na vyama vya mrengo wa kushoto na upinzani.

Michel, ambaye aliingia madarakani mnamo 2014 alipoteza uungwaji mkono na chama chake (N-VA) kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa wa uhamiaji.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana