Hatua hii imekuja, baada ya Waziri Mkuu May kuahirisha upija kura wa kuunga au kukata mkataba wa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, hadi tarehe 14 mwezi Januari.
Corbyn, amesema haikubaliki kwa Waziri Mkuu kuchelewesha upigaji kura na kumlaumu kwa kuiweka nchi hiyo kwenye mzozo.
Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa serikali haitatenga muda kwa muswada huo kujadiliwa.