Pata taarifa kuu
UFARANSA-SHAMBULIZI-USALAMA

Wanne wauawa katika shambulizi Strasbourg, Ufaransa

Watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine kumi na wawili kujeruhiwa katikati mwa mji wa Strasbourg. Tukio hilo lilitokea Jumanne usiku katika eneo lililo karibu na soko la Krismasi mashariki mwa mji wa Strasbourg, nchini Ufaransa.

Askari karibu na soko la Krismasi huko Strasbourg, ambapo watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi Jumanne jioni Desemba 11, 2018.
Askari karibu na soko la Krismasi huko Strasbourg, ambapo watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi Jumanne jioni Desemba 11, 2018. REUTERS/Vincent Kessle
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya wanne wameuawa na wengine 12 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Christophe Castaner, ambaye ametangaza kuwa nchi hiyo inapitia sasa kipindi cha "shambulizi la dharura".

Watu sita kati ya waliojeruhiwa wameelezwa kuwa katika hali mbaya.

Polisi bado inaendelea na operesheni kabambe mjini Strasbourg baada ya mshambuliaji kufyatua risasi dhidi ya umati wa watu katika eneo la kitalii la mji huo. Ubadilishanaji tisasi ulitokea kati ya vikosi vya usalama na mshambuliaji. Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Les Dernières Nouvelles d'Alsace, polisi iliendesha operesheni katika jengo moja la eneo la Neudorf, lakini mshambuliaji bado hajapatikana.

Kwa mujibu wa waziri wa Mambo ya Ndani, Christophe Castaner, shambulio hilo limegharimu maisha ya watu watatu na wengine kumi na wawili kujeruhiwa. Lakini kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Meya wa jiji hilo, watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine kumi na wawili wamejeruhiwa.

"Mshambuliaji anajulikana," amesema Waziri wa Mambo ya Ndani Christophe Castaner, ambaye aliwasili katika eneo la tukio usiku wa manane. Mshambuliaji, mwenye umri wa miaka 29, anayehafamika kwa herufi S, kwa usalama wa taifa, alizaliwa huko Strasbourg, na anajulikana kwa makosa mbalimbali.

Polisi wanasema mshukiwa wa tukio hilo, tayari anajulikana na vyombo vya ulinzi na kuna uwezekano wa kuwa ni tukio la kigaidi.

Shambulio hili limejiri siku chache tu tangu nchi hiyo ishuhudie maandamano mabaya zaidi kupinga Sera za rais Emmanuel Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.