Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAANDAMANO-USALAMA-UCHUMI

Maandamano Ufaransa: Emmanuel Macron kulihutubia taifa Jumatatu hii

Siku mbili baada ya maandamano mapya yanayoendelea nchini Ufaransa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kulihutubia taifa Jumatatu hii, Desemba 10. Kabla ya hotuba yake, atawapokea viongozi mbali mbali waliochaguliwa na washirika wa kijamii katika ikulu ya Elysée.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Elysée tarehe 2 Desemba 2018.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Elysée tarehe 2 Desemba 2018. REUTERS/Stephane Mahe/Pool
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kumuachia nafasi Waziri Mkuu Edouard Philippe kukabiliana na hali hiyo kufuatia hasira ya waandamanaji, Emmanuel Macron anajiandaa kukabiliana na hali hiyo mwenyewe. Rais "atalihutubia taifa" Jumatatu hii saa mbili usiku, Ikulu ya Elysee imesema katika taarifa yake, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi. Rais Macron hajazungumza tangu Desemba 1, baada ya mkutano wa nchi zilizostawi kiuchumi (G20) huko Buenos Aires.

Siku mbili baada ya maandamano mapya ambapo walishiriki watu 136,000 nchini Ufaransa, wanasiasa mbali mbali kwa jumla wanamuomba rais wa jamuhuri kutoa hotuba itakayokidhi madai ya waandamanaji na kukomesha maandamanaji hayo.

"Rais anahitaji kuongea, aongee haraka, atoe hotuba itakayokidhi mada ya waandamanaji" Meya wa mji wa Bordeaux Alain Juppé amesema.

Tangu maandamano hayo yalipoanza wiki tatu zilizopita, machafuko yameongezeka kwa kasi kila kunapoteokea maandamano katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambako kulitokea machafuko makubwa siku ya Jumamosi wiki mbili zilizopita.

Kufuatia kuzuka kwa mgogoro uliosababishwa na waandamaji wanaopinga kuongezwa kwa kodi ya mafuta nchini Ufaransa, serikali imesema iko tayari kuachana moja kwa moja na hatua ya kupandisha kodi ya bidhaa hiyo kama hakutapatikana "ufumbuzi mzuri."

Kwa sasa, ongezeko la kodi ya mafuta imefutwa, alitangaza Waziri wa Mazingira François de Rugy.

"Kama hatutapata ufumbuzi sahihi, hatuna dudi kuachana na hatua hiyo, " alisema Waziri Mkuu. Hatutatekeleza hatua ya" ongezeko la kodi ya mafuta iliyopangwa Januari 1, hatua ambayo ilizua sintofahamu na kusababisha maandamano ya kila kukicha, " aliongeza Edouard Philippe.

Lakini ongezeko la kodi ya mafuta iliyopangwa kuanza kutumika Januari 1, 2019 "imefutwa kwa mwaka 2019," alisema kwa upande wake Waziri wa Mazingira François de Rugy kwenye televisheni ya BFM TV.

Hatua hii imekuja, baada ya maandamano ya wiki mbili kupinga nyongeza hiyo na kusabisha mali na makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa Polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.