Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Ufaransa: Wizara ya Mambo ya ndani yaandaa kwa ulinzi mkali hatua ya 4 ya waandamanaji

media Kitengo cha polisi tarehe 1 Desemba 2018 mbele ya Arc de Triomphe Paris wakati wa maandamano ya kupinga kodi ya mafuta. REUTERS/Stephane Mahe/

Siku moja kabla ya hatua ya 4 ya waandamanaji, Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Ufaransa imeweka hatua ya mwisho kwenye mkakati wake wa kuimarisha usalama kwa siku ya Jumamosi.

Ulinzi umeimarishwa katika maneo mablimbali nchini Ufaransa, makumbusho na maduka ya Champs Elysees yafungwa. Mamlaka nchini Ufaransa inajiandaa kwa kuzima machafuko ambayo yanaweza kujitokeza kufuatia maandamano hayo.

Tangu maandamano hayo yalipoanza wiki tatu zilizopita, machafuko yameongezeka kwa kasi kila kunapoteokea maandamano katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ambako kulitokea machafuko makubwa siku ya Jumamosi.

Kufuatia kuzuka kwa mgogoro uliosababishwa na waandamaji wanaopinga kuongezwa kwa kodi ya mafuta nchini Ufaransa, serikali imesema iko tayari kuachana moja kwa moja na hatua ya kupandisha kodi ya bidhaa hiyo kama hakutapatikana "ufumbuzi mzuri."

Kwa sasa, ongezeko la kodi ya mafuta imefutwa, alitangaza Waziri wa Mazingira François de Rugy.

"Kama hatutapata ufumbuzi sahihi, hatuna dudi kuachana na hatua hiyo, " alisema Waziri Mkuu. Hatutatekeleza hatua ya" ongezeko la kodi ya mafuta iliyopangwa Januari 1, hatua ambayo ilizua sintofahamu na kusababisha maandamano ya kila kukicha, " aliongeza Edouard Philippe.

Lakini ongezeko la kodi ya mafuta iliyopangwa kuanza kutumika Januari 1, 2019 "imefutwa kwa mwaka 2019," alisema kwa upande wake Waziri wa Mazingira François de Rugy kwenye televisheni ya BFM TV.

Hatua hii imekuja, baada ya maandamano ya wiki mbili kupinga nyongeza hiyo na kusabisha mali na makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa Polisi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana