Uingereza yataka heshima kutoka kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya
Waziri Mkuu wa Uingereza Teresia May ameitaka Umoja wa Ulaya, kuiheshimu nchi yake wakati huu majadiliano yakiendelea kuhusu namana nchi hiyo itakavyojiondoa kwenye Umoja huo.
Imechapishwa:
May amesema viongozi wa Umoja huo kukataa mpango wake wa namna Uingereza itakavyojiondoa katika Umoja huo, kuhusu masuala ya biashara, ajira na mipaka ni suala ambalo halikubaliki.
Uigereza inatarajiwa kujiondoa kabisa katika Umoja huo kufikia tarehe 29 mwezi Machi mwaka ujao kwa mujibu wa mkataba uliounda Umoja huo.
Rais wa Baraza hilo Donald Tusk amesema yupo tayari kuendelea kuzungumza na Uingereza na badala yake kusema Waziri Mkuu May ndiye anayeonesha ugumu katika mazungumzo haya.
Uingereza imetishia kujiondoa katika mazungumzo hayo iwapo haitasikilizwa.