Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-SIASA

Scott Morrison ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya Australia

Chama cha Liberal nchini Australia, kimemteua Scott Morrison kuwa Waziri Mkuu mpya kuchukua nafasi ya Malcolm Turnbull. Turnbull alikuwa kwenye shinikizo kubwa kuanzia kuorodheshwa katika kura za kutafuta maoni.

Scott Morrison ambaye ndiye mweka hazina wa sasa alishinda kura 45 kati ya 50 dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton amesema kinara wa chama cha kiliberali, Nola Maroni
Scott Morrison ambaye ndiye mweka hazina wa sasa alishinda kura 45 kati ya 50 dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton amesema kinara wa chama cha kiliberali, Nola Maroni AFP PHOTO / William WEST
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na mzozo wa uongozi wa chama hicho, viongozi wa chama waliamua kuitisha Uchaguzi na kumchagua Morrison ambaye ni Mwekahazina aliyepata kura 45 huku mpinzani wake Peter Dutton akipata kura 40.

Scott Morrison anakuwa Waziri Mkuu wa 30 katika taifa hilo ambalo limeendelea kushuhudia mzozo wa uongozi ndani ya miaka 10.

Morrison ambaye alishinda kura 45 kati ya 50 dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton amesema kinara wa chama cha kiliberali Nola Maroni.

Hata hivyo Bw Turnbull hakuwania katika ushindani huo wa uongozi.

Turnbull alikuwa akipuuzia wito wa kumtaka ajiuzulu wakati tuhuma za uongozi zikiididimiza serikali yake.

Morrison aliwahi kuwa mkurugenzi msimamizo wa utalii Autralia ambaye ameshikilia wizara kadhaa zikiwemo za uhamiaji na huduma kwa jamii.

Alipata umaarufu kitaifa alipokuwa waziri wa uhamiaji katika serikali ya waziri mkuu wa zamani Tony Abbott.

Alijenga sifa ya kuwa kiongozi asiyetaka upuuzi katika kuidhinisha sera kali ya Australi ya kusitisha uhamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.