Waokoaji waendelea kutafuta watu waliokwama Genoa Italia
Shughuli ya uokoaji inaendelea huko Genoa, kaskazini mwa Italia, baada ya kuvunjika kwa daraja la barabara ya mwendo kasi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30. Waziri wa usafirishaji Danilo Toninelli ameliongelea janga hilo kuwa kubwa.
Imechapishwa:
Magari zaidi ya 30 yalianguka katika upande wa mfereji wa uchafu.
Wafanyakazi wa dharura wanajaribu kuwatafuta watu walioanguka na magari yao huku wakiwa wanasaidiana na mbwa wenye utaalamu kwa kunusa.
Sauti za kuomba msaada kutoka kwa watu wanaosadikiwa kunaswa katika mabaki ya daraja hilo zimesikika usiku kucha.
Ufaransa imehaidi kushirikiana pamoja na Italia katika janga hilo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameandika ujumbe wa pole katika ukurasa wake wa Twitter kwa raia wa Italia na Ufaransa.
I nostri pensieri vanno alle vittime, ai loro familiari e a tutto il popolo italiano. La Francia è vicina all’Italia in questa tragedia e rimane pronta ad apportare tutto il sostegno necessario. #Genova #Gêneshttps://t.co/A7YAfnK3AY
Emmanuel Macron (@EmmanuelMacron) August 14, 2018
Daraja hilo ambalo lilijengwa tangu mwaka 1960,l ilikuwa linawahudumia raia wa Italia na Ufaransa.
Naibu waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo ,Edoardo Rixi amesema idadi ya vifo ni 35 lakini wanatarajia kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.