Pata taarifa kuu
URENO-USALAMA-MAJANGA ASILI

Ureno yakumbwa na mkasa wa moto, ishirini na tano wajeruhiwa

Zaidi ya maafisa 1,150 wa Zima Moto wametumwa Jumatatu wiki hii kujaribu kuzima moto unaoendelea kusambaa tangu Ijumaa wiki iliyopita katika mkoa wa Algarve, kusini mwa Ureno.

Moto wajeruhi watu ishirini na tano Ureno, watu kadhaa na watalii waondolewa katika mkoa wa Algarve, kusini mwa nchi.
Moto wajeruhi watu ishirini na tano Ureno, watu kadhaa na watalii waondolewa katika mkoa wa Algarve, kusini mwa nchi. REUTERS/Rafael Marchante
Matangazo ya kibiashara

Moto huo uliwajeruhi watu 25 usiku wa Ijumaa na kusababisha wakaazi wa maeneo kadhaa ya mkoa huo na watalii kuondolewa na kupelekwa maeneo salama.

Upepo mkali unaotoka katika eneo la Sahara na ukame vinasababisha moto huo kusambaa haraka katika maeneo mbalimbali. Joto limeanza kupanda kwa kiwango cha juu katika sehemu nyingi za nchi.

Idara ya huduma za dharura iliwaweka tayari maafisa 350 wa ziada wa Zima Moto ili kukabiliana na moto huo usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

Watu ishirini na wanne wanaendelea kuuguza majeraha madodo madogo yaliyosababishwa na moto au kukosa pumzi kutokana na moshi mwingi. Mwathirika wa 25 ana majeraha makubwa.

Ni vigumu kwa idara ya Zima Moto kuendelea na shughuli yao katika maeneo yaliyoathirika na mkasa huo wa moto kutokana na moshi ambao mkubwa unaoendelea kufumba katika maeneo hayo, idara ya huduma za dharura imesema, huku ikibaini kwamba helikopta tisa pia zishiriki katika zoezi hilo.

Moto ulizuka siku ya Ijumaa katika eneo la hifadhi ya Monchique, maarufu kwa watalii.

Ureno bado inakubukumbuka mikasa miwili ya moto mkubwa ambayo iliua watu 114 mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.