Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA-UHURU-MACRON

Ufaransa yaadhimisha miaka 229 ya mapinduzi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameongoza maadhimisho ya miaka 229, tangu kutokea kwa mapinduzi nchini humo maarufu kama Bastile.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa maadhimisho ya siku ya mapinduzi Julai 14 2018 jijini Paris
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa maadhimisho ya siku ya mapinduzi Julai 14 2018 jijini Paris rf
Matangazo ya kibiashara

Ni siku ambayo raia wa Ufaransa wanakumbuka namna jeshi lao lilifanikisha harakati za kumaliza uongozi wa Kifalme na kuundwa na Jamhuri ya Ufaransa na kubadilisha mfumo wa uongozi na kuwaachilia wafungwa.

Wanajeshi wakiwa kwenye gwaride, pamoja na ndege za kivuta na magari, zimetumiwa kama kumbukumbu ya siku hii inayoadhimishwa kila tarehe 14 mwezi Julai.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, ambaye alikuwa amealikwa katika maadhimisho ya mwaka huu, hakufanikiwa kufika kwa sababu ya mafuriko katika nchi yake lakini aliwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya nje Taro Kono.

Maadhimisho ya mwaka huu yamekuja, wakati huu timu ta taifa ya Ufaransa ikijiandaa kucheza na Croatia katika fainali ya kombe la dunia nchini Urusi, siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.