Pata taarifa kuu
MAREKANI-UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-UCHUMI

Donald Trump aionya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Uingereza haitaingia mkataba wa kibiashara na Marekani ikiwa mpango wa waziri mkuu kujitoa katika Umoja wa Ulaya utaendelea.

Theresa May anasema yuko tayari kumueleza Trump kuhusu mpango wake wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Theresa May anasema yuko tayari kumueleza Trump kuhusu mpango wake wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Uingereza amekuwa akijitahidi kutumia ziara hii ya kwanza ya Trump kumshawishi kuhusu biashara huru kati ya mataifa hayo mawili akibaini kwamba suala la kujiotoa katika Umoja wa Ulaya ni fursa ya kukukuza uchumi kati ya Marekani na Uingereza.

Hata hivyo Donald Trump amesema kuwa alimshauri Bi.May njia nzuri ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya lakini hakuweza kumsikiliza.

“Hatuwezi kuwa tayari kuwa na ushirikiano ambao ndani yake kuna Umoja wa Ulaya, “ amesema rais wa Marekani.

“Lengo la Marekani ni kufanya biashara na Uingereza pekee bila kuhusisha umoja wa Ulaya, “ ameongeza rais Trump.

Katika mahojiano na gazeti la Sun, rais Donald Trump amesema “mpango wa waziri mkuu wa Uingereza utaua mipango ya kibiashara kati ya Uingereza na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.