Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-KANISA-HAKI

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Australia afungwa jela miezi 12

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Australia, amefungwa jela miezi 12 kwa kutoripoti kesi za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto miaka 1970, zilizofanywa na kasisi wa Kanisa hilo.

Philip Wilson (katikati), Askofu Mkuu wa Adelaide, kusini mwa Australia akiwasili katika mahakama ya Newcastle, Mei 22, 2018.
Philip Wilson (katikati), Askofu Mkuu wa Adelaide, kusini mwa Australia akiwasili katika mahakama ya Newcastle, Mei 22, 2018. AAP/Peter Lorimer/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Philip Wilson, amepatikana na kosa hilo na anakuwa mmoja wa viongozi wa Kanisa hilo duniani ambaye amepatikana na kosa hilo.

Mahakama hata hivyo, imesema kuwa Askofu huyo atazuiwa nyumbani kwa muda huo wote.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Australia alijiuzulu baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya kuficha kashfa za ulawiti iliyokuwa ikimuandama.

Philip Wilson, Askofu Mkuu wa Adelaide, kusini mwa Australia anakuwa afisa wa kwanza wa ngazi za juu wa Kanisa Katoliki kushtakiwa na kuhukumiwa kutokana na kashfa za ngono zinazolizunguka kanisa hilo kwa miongo mingi sasa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.