Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Umoja wa Ulaya waafikiana kuhusu masuala ya wahamiaji

media "Hatua zote zilizochukuliwa kuhusiana na vituo vitakavyodhibitiwa, ikiwa ni pamoja na kuhamishwa na kupelekwa sehemu nyingine vitafanyika kwa hiari," imesema taarifa iliyosainiwa na viongozi wa Ulaya baada ya saa tano za majadiliano. REUTERS/Stéphanie Lecocq

Baada ya saa kadhaa za majadiliano, hatimaye viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana huko Brussels wameafikiana kuhusu masuala ya wahamiaji na hivyo kuepukana na mgogoro mpya.

Italia imekua imezuia tangu Alhamisi jioni wiki hii kupitishwa kwa maazimio ya pamoja katika mkutano wa Umoja wa Ulaya wa Brussels, kwa kuomba nchi nyingine kujibu kwanza madai yake kuhusu suala la wahamiaji, hali ambayo ilitaka kuzua mgawanyiko mkubwa ndani ya Umoja wa Ulaya.

"Hatua zote zilizochukuliwa kuhusiana na vituo vitakavyodhibitiwa, ikiwa ni pamoja na kuhamishwa na kupelekwa sehemu nyingine vitafanyika kwa hiari," imesema taarifa iliyosainiwa na viongozi wa Ulaya baada ya saa tano za majadiliano.

Nchi hizo ishirini na nane za Umoja wa Ulaya pia zimeamua kuidhibiti mipaka yao ya nje, hasa kwa kuiongezea misaada Uturuki na Afrika Kaskazini, ili kuepuka kurudi kwa wimbi la wahamiaji na wakimbizi sawa na lile lililoshuhudiwa Ulaya mnamo mwaka 2015.

Taarifa hiyo inaonyesha pia kuwa mfumo wa kuanzishwa kwa "vituo vya mapokezi" vinavyopatikana nje ya eneo la Ulaya utafadhiliwa. Viongozi wa Ulaya pia wamekubaliana juu ya kuundwa kwa "vituo vitakavyodhibitiwa" ambapo yatajadiliwa maombi kuhusu hifadhi ya ukimbizi yatakayowasilishwa na wakimbizi.

Rais wa serikali ya Italia Giuseppe Conte, amekaribisha matokeo ya mkutano huo na kusema kuwa Italia haiko "peke yake". Roma itaamua baadaye ikiwa ni lazima au la kuwa na vituo vya mapokezi kwa wahamiaji, ameongeza.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizungumzia "nia ya kulinda vema mipaka na kuimarisha sheria za mapokezi".

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana