Pata taarifa kuu
UTURUKI-UCHAGUZI

Uchaguzi Uturuki: Rais Erdogan kwenye mtihani mkubwa wa kusalia madarakani

Wananchi wa Uturuki wamepiga kura Jumapili hii kuchagua wabunge na rais katika uchaguzi ambao unatajwa kuwa kipimo cha juu kwa rais Recep Tayyip Erdogan wakati huu upinzani wakitumia hali mbaya ya uchumi wa taifa hilo kupata umaarufu.

Mwananchi wa Uturuki akipiga kura kwenye uchaguzi wa kwanza ambao wapiga kura watachagua wabunge na rais, 24.06.2018
Mwananchi wa Uturuki akipiga kura kwenye uchaguzi wa kwanza ambao wapiga kura watachagua wabunge na rais, 24.06.2018 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Erdogan ameshuhudia mabadiliko makubwa ya nchi hiyo tangu chama tawala cha kiislamu kiingie madarakani mwaka 2002 baada ya miongo kadhaa ya utawala wa kidini.

Hata hivyo wakosoaji wake wanamtuhumu Erdogan mwenye umri wa miaka 64 hivi sasa kwa kuminya uhuru wa watu kutoa maoni na kuonesha makucha ya kuwa mtawala wa kiimla.

Macho yote yakiwa kwenye uwazi wa kura yenyewe, vituo vilifunguliwa mapema alfajiri na vilitarajiwa kufungwa majira ya jioni na matokeo ya awali kutarajiwa kuanza kutolewa usiku.

Kukiwa na idadi ya watu milioni 56 wenye haki ya kupiga kura, kwa mara ya kwanza wanapiga kura sambamba kuchagua wabunge na rais, huku rais Erdogan akitarajiwa kushinda kwenye duru ya kwanza na chama chake kupata ushindi wa jumla.

Hata hivyo mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Republican People's, Muharrem Ince amefanikiwa kupata idadi kubwa ya wahudhiriaji kwenye mikutano yake ya kampeni anatarajiwa kupata idadi kubwa ya viti bungeni.

Erdogan bado anatarajiwa kushinda hata kama uchaguzi huu utaenda kwenye duru ya pili Julai 8.

Wadadisi wa mambo wanasema upinzani safari huu licha ya kutokuwa na nguvu iliyotarajiwa lakini wametoa tishio kubwa kwa utawala wa rais Erdogan ambaye akishinda anatarajiwa kufuta nafasi ya waziri mkuu na kuwa kiongozi mwenye madaraka makubwa zaidi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.