Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Ufaransa yaishtumu Italia kukataa kuwapokea wahamiaji

media Wahamiaji 629, ikiwa ni pamoja na watoto wengi na wanawake, wamepata msaada kutoka kwa meli ya Aquarius, meli ya shirika la kihisani la SOS Méditerranée, katika pwani ya Mediterania, Juni 10, 2018. Reuters

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameishutumu Serikali ya Italia kwa kutowajibika baada ya nchi hiyo kukataa kuwapokea wahamiaji na kuwaacha kwenye sintofahamu katika meli iliyokuwa imewaokoa kwenye bahari ya Mediterania.

Meli ya Aquarius ambayo imebeba wahamiaji 629 itasindikizwa na meli nyingine mbili za jeshi la wanamaji wa Italia kuwapelekea wahamiaji hao nchini Uhispania kwenye mji wa Valencia ambako Serikali imekubali kuwapokea.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian ametupilia mbali madai kuwa nchi yake imekuwa ikikwepa kuwapokea wahamiaji na kuiachia Italia peke yake.

Haya yanajiri wakati huu maelfu ya wahamiaji wakiendelea kufanya safari za hatari kupitia bahari ya mediterania kuingia barani Ulaya kutafuta maisha na nchi ya Italia imekuwa kituo chao kikuu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana