Pata taarifa kuu
UHISPANIA-WAHAMIAJI

Uhispania yakubali kupokea wahamiaji waliokwama katika meli baharini

Uhispania imekubali kupokea wahamiaji 629 waliokwama katika meli moja ya shirika la kihisani ya Aquarius iliyokataliwa kutia nanga nchini Italia na Malta, serikali ya Pedro Sanchez imesema katika taarifa yake.

Meli iliyokua ikibeba wahamiaji 629 imeruhusiwa kutia nanga nchini Uhispania.
Meli iliyokua ikibeba wahamiaji 629 imeruhusiwa kutia nanga nchini Uhispania. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Meli ya Aquarius imeruhusiwakutia nanga katika bandari ya Valencia, pwani ya mashariki ya Uhispania, ofisi ya waziri mkuu wa Uhispania imesema.

Meli hiyo ilikua imeegesha katika ya bahari kati ya Italia na Malta ikiwa imebeba wahamiaji 629 ikiwa ni pamoja na watoto 123 wasiokuwa wasiokuwa na wazazi, watoto wengine kumi na mmoja na wanawake saba wajawazito.

Serikali ya Italia meli hiyo kutua nanga katika ardhi yake na kuomba Malta kuipokea.

"Malta haipokei mtu yeyote, Ufaransa inawafukuza watu mpakani, Uhispania inalinda mipaka yake kwa kutuma jeshi lake, na kuanzia hivi leo, Italia pia meanza kusema hapana kwa biashara ya binadamu, hatutaki wahamiaji haramu, "aliandika Jumapili kwenye ukurasa wake wa Facebook Matteo Salvini, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia.

Wahamiaji zaidi ya 600,000 wamewasili nchini Italia kwa meli tangu mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.