Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Hatma ya waziri mkuu wa Uhispania kujulikana Ijumaa

media Waziri Mkuu wa Hispania Mariano Rajoy, Madrid Mei 31, 2018. REUTERS/Susana Vera

Bunge la Uhispania linatarajia Ijumaa wiki hii kupiga kura ya kutokua na imani na kiongozi wa serikali Mariano Rajoy. Bw Rajoy anaona kuwa shinikizo la upinzani limeongezeka baada ya chama cha Popular Party (PP, cha mrengo wa kulia) kujikuta matatani katika kesi ya rushwa.

Kura ya kutokua na imanani na kiongozi wa serikali ya Uhispania iliyowasilishwa wiki iliyopita na chama cha Kisoshalisti cha PSOE ilijadiliwa siku ya Alhamisi wiki hii na inatazamiwa kupigiwa kura Ijumaa wiki hii wakati ambapo wito wa uchaguzi wa wabunge wa mapema ulikua ukiendelea.

Ili kuiangusha serikali, upinzani unahitaji kwa uchache kura 176 bungeni. Jambo ambalo ilishindwa kufanikisha katika kura nyingine ya kutokua na imani na kiongozi wa serikali mnamo mwezi Juni mwaka jana.

Chama cha mrengo wa kati cha Ciudadanos (Wananchi), kilisema siku ya Jumamosi kuwa kiko tayari kushirikiana na chama chama cha PSOE kuunga mkono mgombea huru atakayechukua nafasi ya Mariano Rajoy, ambaye serikali tayari inakabiliwa na udhaifu kutokana na mgogoro wa Catalonia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana