Pata taarifa kuu
UBELGIJI-USALAMA

Watu watatu wauawa kwa kupigwa risasi Ubelgiji

Watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Liege, nchini Ubelgiji. Askari wawili na mwanamke wameuawa na mtu mwenye silaha ambaye pia alimshikilia mateka mtu mmoja kabla ya kuuawa na vikosi vya usalama.

Eneo la shambulizi huko Liège, Jumanne, Mei 29, 2018.
Eneo la shambulizi huko Liège, Jumanne, Mei 29, 2018. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea saa 10:30 asubuhi (saa za Ubelhiji) wakati kwenye barabara kuu ya Avroy. Mshambuliaji alifyatua risasi kwenye umati wa watu, kabla ya kukimbilia katika shule moja la sekondari. Wakati huo watu kadhaa walitekwa nyara, kabla ya vikosi vya usalama kuingilia kati na kufaulu kumua mshambuliaji.

Uchunguzi unaendeshwa na ofisi ya mashitaka, ambayo itachunguza kama kitendo hicho kilikua cha kigaidi.

Kwa mujibu wa chanzo cha polisi, polisi wawili ni miongoni mwa waliouawa.

Mwanamke aliyeuawa alikua akipita na gari lake wakati wa tukio hilo, bila hata hivyo kujua,kwa mujibu wa Catherine Collignon, msemaji wa ofisi ya mashitaka ya Liège. "Bado Hatujajua chochote," ameongeza. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ubelgiji Jan Jambon amesema anasikitishwa na mauaji hayo huku akiomba raia kuwa wa tulivu, wakati huu uchunguzi ukiendelea.

"Kuna mambo ambayo yanaonyesha kuwa kitendo hicho ni cha kigaidi," amesema Eric Van Der Sypt, msemaji wa ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji, wakati ambapo vyombo vya habari vya Ubelgiji vimeanza kukusanya taarifa zaidi kuhusu mshambuliaji.

Ubelgiji ilikumbwa na zimwi la mauaji ya kigaidi mnamo mwezi Machi 2016, ambapo watu 32 waliuawa katika mashambulizi ya kigaidi. Tangu wakati huo nchi hii imeendelea kukabiliwa na mashambulizi kadhaa dhidi ya askari au maafisa wa polisi. Shambulizi la hivi karibuni lililoelezwa kuwa la "kigaidi" lilitokea tarehe 25 Agosti 2017: ni lile la kisu dhidi ya askari mjini Brussels.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.