Pata taarifa kuu
IRELAND-KURA YA MAONI-HAKI

Kura ya maoni kuhusu kuhalalisha utoaji mimba yapigwa Irland

Wananchi huko Ireland wanapiga kura ya maoni Ijumaa wiki hii kura ya maoni ya kihistoria kuamua ikiwa nchi hiyo iunge mkono baadhi ya sheria zinazohalalisha utoaji mimba au la.

Wafuasi wa kura ya "hapana" kwa utoaji mimba, Mei 24 Dublin siku moja kabla ya kura ya maoni juu ya suala hilo nchini Ireland.
Wafuasi wa kura ya "hapana" kwa utoaji mimba, Mei 24 Dublin siku moja kabla ya kura ya maoni juu ya suala hilo nchini Ireland. BARRY CRONIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wanaharakati wanasema si vyema kupitisha sheria ya kuharamisha utoaji wa mimba nchini Ireland na kwa sababu wanawake huwa hawatoi mimba kwa kupenda.

Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu, Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Irland walitoa wito wa kupinga kura ya maoni ya utoaji mimba.

“Ikiwa jamii inakubali kuwa mwanadamu anayo haki ya kumaliza maisha ya mwingine, basi haiwezekani kudai haki ya maisha kama haki ya msingi ya binadamu kwa mtu yeyote”. Haya ni maelezo ya Askofu wa Ireland  Kevin Doran (Elphin) Mwenyekiti wa kikosi cha masomo juu ya elimu ya viumbe wa Tume ya Baraza la Maaskofu katika ujumbe wa kichungaji uliotangazwa tarehe 28 Januari 2018, akirudi katika mada ya utoaji mimba, kwa kusubiri matokeo ya mkutano wa serikali ya nchi ambao, tarehe 29 Januari 2018 ulitarajia kutoa ruhusa ya kwenda mbele katika kupanga tarehe ya kupiga kura ya maoni juu ya suala la utoaji mimba.

Nchi nyingi duniani zinapinga sana vitendo vya ukatili hasa kwa wanawake na watoto lakini baadhi ya nchi zimeanza kulegeza sheria za utoaji mimba na kutaka kuhalalisha sheria hizo na kufanya kuwa zoezi katika jamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.