Pata taarifa kuu
UHISPANIA-CATALONIA-SIASA

Madrid yakataa kuidhinisha serikali ya Catalonia

Serikali kuu ya Uhispania imesema Jumatatu wiki hii kuwa inatambua mamlaka ya rais wa Catalonia aliyechaguliwa hivi karibuni, lakini imekataa kuthibitisha muundo wa serikali ya eneo hilo, na hivyo Madrid kuendelea kuitawala Catalonia.

Rais mpya wa Catalonia Quim Torra akizungukwa na mkewe Carola Miro (kushoto) na Marcela Topor, mke wa rais wa zamani wa jimbo hilo aliyeuhamishoni nchini Ujerumani Carles Puigdemont. Barcelona, Mei 14, 2018.
Rais mpya wa Catalonia Quim Torra akizungukwa na mkewe Carola Miro (kushoto) na Marcela Topor, mke wa rais wa zamani wa jimbo hilo aliyeuhamishoni nchini Ujerumani Carles Puigdemont. Barcelona, Mei 14, 2018. REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Quim Torra, aliyechaguliwa Jumatatu iliyopita kwenye wadhifa wa rais wa Catalonia, alitangaza Jumamosi baraza lake la mawaziri ambalo linaundwa na watu kadhaa wakiwemo watu wanne waliowekwa kizuizini au walio uhamishoni Brussels.

Serikali ya Mariano Rajoy, ambayo iliweka Catalonia chini ya mamlaka yake baada ya kutangazwa uhuru wa eneo hilo Oktoba 27, ameghadhabishwa juu ya kuwepo kwa watu hao wanne kwenye serikali ya jimbo hilo, akitaja kitendo hicho kama cha uchochezi.

Chini ya sheria ya dharura inayofafanua masharti ya usimamizi wa Catalonia, utawala wa moja kwa moja wa eneo hilo hautaondolewa hadi pale serikali ya eneo hilo itaundwa na kukubaliwa.

Mariano Rajoy amesema ana matumaini kuwa Catalonia itaunda haraka serikali nzuri na kuwa tayari kwa mazungumzo ya kina na Madrid.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.