Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
Ulaya

Madrid yakataa kuidhinisha serikali ya Catalonia

media Rais mpya wa Catalonia Quim Torra akizungukwa na mkewe Carola Miro (kushoto) na Marcela Topor, mke wa rais wa zamani wa jimbo hilo aliyeuhamishoni nchini Ujerumani Carles Puigdemont. Barcelona, Mei 14, 2018. REUTERS/Albert Gea

Serikali kuu ya Uhispania imesema Jumatatu wiki hii kuwa inatambua mamlaka ya rais wa Catalonia aliyechaguliwa hivi karibuni, lakini imekataa kuthibitisha muundo wa serikali ya eneo hilo, na hivyo Madrid kuendelea kuitawala Catalonia.

Quim Torra, aliyechaguliwa Jumatatu iliyopita kwenye wadhifa wa rais wa Catalonia, alitangaza Jumamosi baraza lake la mawaziri ambalo linaundwa na watu kadhaa wakiwemo watu wanne waliowekwa kizuizini au walio uhamishoni Brussels.

Serikali ya Mariano Rajoy, ambayo iliweka Catalonia chini ya mamlaka yake baada ya kutangazwa uhuru wa eneo hilo Oktoba 27, ameghadhabishwa juu ya kuwepo kwa watu hao wanne kwenye serikali ya jimbo hilo, akitaja kitendo hicho kama cha uchochezi.

Chini ya sheria ya dharura inayofafanua masharti ya usimamizi wa Catalonia, utawala wa moja kwa moja wa eneo hilo hautaondolewa hadi pale serikali ya eneo hilo itaundwa na kukubaliwa.

Mariano Rajoy amesema ana matumaini kuwa Catalonia itaunda haraka serikali nzuri na kuwa tayari kwa mazungumzo ya kina na Madrid.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana