Pata taarifa kuu
IRAN-EU-MAREKANI

Merkel:Mkataba wa Iran una mapungufu lakini ni muhimu kuulinda

Viongozi wa Umoja wa Ulaya ambao wamekuwa wakikutana jijini Sofia nchini Bulgaria, wamesema wamekubaliana kuwa mkataba wa Iran una mapungufu lakini unastahili kulindwa.

Angela Merkel Kansela wa Ujerumani
Angela Merkel Kansela wa Ujerumani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema, licha ya Marekani kujiondoa, ni vema kwa mataifa yaliyotia saini kuendelea kuulinda mkataba huo wakati mazungumzo yakiendelea kujadili masuala tata kuhusu mradi huo.

"Sisi katika Umoja wa Ulaya, tumekubaliana kuwa mkataba huu una mapungufu lakini tumekubaliana kuulinda," alisema Kansela Merkel.

Mwaka 2015 Iran na mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani yalikubaliana kuwa Tehran iachane na mradi huo kwa miaka 10 na baadaye itumie madini yake ya uranium kwa sababu za kiteknolojia badala ya kutengeza silaha za maangamizi.

Marekani ilijiondoa katika mktaba huo ikisema, ulikuwa unaipa Iran ya kutengeza silaha za maangamizi na hivyo kuendelea kulifanya taifa hilo kuwa hatari kwa usalama wake na ile wa mshirika wake wa karibu wa Iran.

Hatua hii imeikera serikali ya Iran.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.