Pata taarifa kuu
SWEDEN-FASIHI-TUZO YA NOBEL

Tuzo ya Nobel ya Fasihi 2018 yaahirishwa kutokana na kashfa ya ngono

Hakutakuwa na Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka huu. Tangazo lilitolewa Ijumaa asubhi wiki hii, huko Stockholm, na Chuo cha Sweden. Taasisi inayotoa tuzo ya nobel ya fasihi.

Kristina Lugn, mwanachama wa Chuo cha Nobel, alipofika mwezi Mei 3 kwenye makao makuu ya shirika hilo kwa mkutano kati ya wanachama.
Kristina Lugn, mwanachama wa Chuo cha Nobel, alipofika mwezi Mei 3 kwenye makao makuu ya shirika hilo kwa mkutano kati ya wanachama. News Agency/Fredrik Sandberg/via REUTERS.
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hii ilifadhaika kwa miezi kadhaa, kufuatia kufichuliwa kwa visa vya unyanyasaji wa kijinsia na matumizi mabaya ya kifedha katika taasisi hiyo.

Taasisi hiyo ya Sweden imekuwa kwenye mzozo mkali kutokana na namna wanavyoshughulikia shutuma dhidi ya mume wa mfanyakazi wa taasisi hiyo

Taasisi imesema itatangaza mshindi wa mwaka 2018 na mshindi wa mwaka 2019 mwakani.

Uamuzi huu wa kuahirisha Tuzo ya Nobel ya Fasihi, ambayo haijawahi kuchukuliwa tangu mwaka 1949, ni matokeo ya yanayoikabili taasisi hiyo inayotoa tuzo ya nobel ya fasihi.

Mgawanyiko ulianza kujitokeza mwezi Novemba mwaka jana baada ya mpiga picha raia wa Ufaransa Jean-Claude Arnault aliyekuwa akifanya kazi ya kuongoza mradi wa maswala ya tamaduni uliokuwa ukifadhiliwa na shule ya Sweden, alikuwa akishutumiwa kuwadhalilisha kingono wanawake 18.

Wanawake kadhaa kati yao waliripoti kuwa vitendo hivyo vilifanyika kwenye maeneo yanayomilikiwa na shule hiyo. Hata hivyo Jean-Claude Arnault amekana shutuma hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.