Pata taarifa kuu
UFARANSA-SYRIA-MACRON

Rais wa Ufaransa atetea mwaka mmoja uongozini

Katika mahojiano kwenye baadhi ya vituo vya habari vya Ufaransa BFMTV, RMC na Mediapart siku ya Jumapili Aprili 15, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema katika mwaka mmoja wa uongozi wake kumeshuhudiwa mageuzi makybwa ambayo yamefanyika kwa kasi na kwa bidii. Rais Macron alijibu, moja kwa moja na maswali ya Jean-Jacques Bourdin na Edwy Plenel kwa karibu saa mbili.  

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron www.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Haya ni mahojiano ya pili kwa vyombo vya habari baada ya yale yaliyofanyika kwenye kituo cha habari cha TF1 katika shule ya Orne siku ya Alhamisi wiki iliyopita.

Siku moja baada ya mashambulizi ya pamoja (Ufaransa - UMarekani - Uingereza) dhidi ya serikali ya Syria, na wakati ambapo serikali ya Ufaransa inakabiliwa na migogoro kadhaa ya kijamii (SNCF, vyuo vikuu ...), Emmanuel Macron alisema kwa mwaka mmoja wa uongozi wake kumeshuhudiwa mageuzi makubwa yaliyofanyika kwa bidii.

Alipoulizwa kuhusu ushahidi wa mashambulizi ya kemikali nchini Syria, rais Macron kwanza alisema kuwa "operesheni ilifanyika kikamilifu. "Makombora yote yamefikia malengo yao na uwezo wa uzalishaji wa silaha za kemikali uliharibiwa.

Emmanuel Macron alisema "kuwa na uthibitisho kupitia vyombo vya usalama [idara ya Ujasusi]" kwamba silaha za kemikali zilitumiwa, na kwamba matumizi haya "yalihusishwa serikali ya Syria".

Kwa swali la kwa nini walitumia mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Rais wa Ufaransa alithibitisha kwamba "ni jumuiya ya kimataifa iliyoingilia kati" akisema kuwa "Ufaransa haijatangaza "vita dhidi ya utawala" wa Bashar al-Assad.

Emmanuel Macron pia alisema anataka "kushawishi" Urusi na Uturuki kuja kwenye meza ya mazungumzo, huku akidai kuwa alimshauri rais wa Marekani Donald Trump, ambaye hivi karibuni alisema kuhusu uwezekano wa kuondoa askari wa Marekani nchini Syria, ili " wanajeshi wa nchi yake waendelee kuwa nchini Syria kwa muda mrefu zaidi ".

Rais Emmanuel Macron hatimaye alithibitisha kwamba atazuru Saint Petersburg mwishoni mwa Mei wakati wa mkutano kuhusu uchumi.

Alipoulizwa kuhusu kuongezeka kwa maandamano nchini Ufaransa (wafanyakazi wa reli, wanafunzi, Notre-Dame-des-Landes), rais alisema "anaelewa" hasira za waandamanaji, lakini anaamini kuwa "hasira haziwezi kusababisha uharibifu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.