Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Kiongozi wa zamani wa Catalonia aachiliwa huru kwa dhamana Ujerumani

media Rais wa zamani wa Catalania Carles Puigdemont wakati wa mahojiano huko Brussels tarehe 23 Desemba 2017. REUTERS/Eric Vidal

Rais wa zamani wa eneo la Catalonia aliyetimuliwa Carles Puigdemond ameachiliwa huru na vyombo vya sheria vya ujerumani, baada ya kukamatwa hivi karibuni kwenye mpaka wa nchi hiyo na Denmark.

Hatua hiyo ilichukuliwa siku ya Alhamisi jioni na mahakama ya Ujerumani baaad ya kufutilia mbali shutma za uasi zilizokua zikimkabilii Bw Puigdemond.

Kiongozi huyo wa zamani wa Catalonia alikamatwa tarehe 25 Machi kaskazini mwa Ujerumani wakati ambapo alikua akitokea Finland akielekea Ubelgiji.

Polisi ya Ujerumani katika kutekeleza hukumu ya baraza zima la Ulaya iliyotolewa na mahakama ya juu ya Uhispania, ilimkamata na kumtia mbaroni Carles Puigdemont, aliyetimuliwa mamlakani na kisha kulazimika kutoroka Uhispania.

Ameachiliwa huru kwa dhamana ya euro 75,000.

Carles Puigdemont ataachiliwa rasmi leo Ijumaa, Aprili 6. Kiongozi huyo wa zamani wa Catalonia anaweza kuondoka jela la Neumünster kaskazini mwa Ujerumani baada ya kulipa euro 75,000. Hana haki ya kuondoka Ujerumani, na ametakiwa kufahamisha mamlaka husika kuhusu harakati zake na kuripoti kwa mamlaka husika mara moja kwa wiki.

Carles Puigdemont anakabiliwa na kifungo cha miaka 25 jela iwapo atarejeshwa nchini Uhispania.

Ni takriban miezi sita sasa imepita tangu Puigdemont alipotoa tangazo la upande mmoja la kujitenga jimbo hilo la Catalonia na maeneo mengine nchini Uhispiania. Kiongozi huyo alituhumiwa kuzusha ghaisa, fitina na uasi wa sheria, na kutakiwa kuripoti mbele ya mahakama ya juu ya nchi hiyo.

Hata hivyo kabla ya kufika mahakamani hapo, alikimbilia nchini Ubelgiji. Kwa ajili hiyo, kutiwa mbaroni mwanasiasa huyo, ni pigo kubwa kwa harakati ya kutaka kujitenga jimbo la Catalania.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana