Carles Puidgemont likamatwa Machi 25 katika katika eneo la kaskazini mwa Ujerumani, wakati alipokua akirejea Brussels, nchini Ubelgiji, baada ya kutembelea Finland. tangu wakati huo anaendelea kushikiliwa katika mji wa Neumünster.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, ofisi ya mashitaka imesema kuwa mashtaka kuhusu hasa kufanyika kwa kura ya maoni iliyodaiwa kinyume cha sheria na serikali kuu ya Uhispania, wakati ambapo kulikua na hofu ya kutokea machafuko, yanakubaliwa kwa sheria ya Ujerumani.
Ikizingatiwa kwamba kiongozi huyo wa zamani wa Catalonia anaweza kutafuta njia ya kuondoka nchini ujerumani, ofisi ya mashitaka imeomba Mahakama Kuu ya mkoa wa Schleswig-Holstein, ambayo itatoa uamuzi wake kuhusu kusafirishwa kwa Carles Puidgemont nchini Uhispania, kumbakiza kizuizini wakati utaratibu wa kisheria ukiendelea.