Pata taarifa kuu
UINGEREZA-URUSI

Uingereza yapongeza kufukuzwa kwa wanadiplomasia wa Urusi

Nchi ya Uingereza Jumanne ya wiki hii imepongeza kile ilichosema hatua ya mataifa ya Ulaya na Marekani kuwafukuza kwenye nchi zao waliotajwa kuwa majasusi za Urusi zaidi ya 100, ikisema huu ni uelekeo mpya wa nchi za magharibi dhidi ya Urusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bortis Johnsonakiwasili kuhudhuria mkutano wa baraza la usalama kwenye ofisi za Downing Street.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bortis Johnsonakiwasili kuhudhuria mkutano wa baraza la usalama kwenye ofisi za Downing Street. REUTERS/Simon Dawson
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Uingereza inatolewa wakati huu Urusi yenyewe ikiahidi kulipa kisasi kutokana na uamuzi uliochukuliwa na mataifa hayo.

Nchi ya Ireland imekuwa ni taifa jingine ambalo limetangaza kuwafurusha wanadiplomasia wa Urusi, wakati huu mpaka sasa wanadiplomasia wa Urusi 117 wamefukuzwa kutoka kwenye matiafa 24 katika muda wa siku 2.

Wadadisi wa mambo wanasema hatua hii inakumbusha wakati wa vita vya baridi ambapo mataifa mengi yalikuwa yanatuhumiana kutuma majasusi kufanya upelelezi na baadae kupelekea kufukuzwa.

“Haijawahi kushuhudiwa hapo kabla kwa nchi kuja pamoja kuwafurusha wanadiplomasia wa Urusi,” amesema waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson katika ukurasa wa maoni yake kwenye gazeti la The Times daily, akisema ni pigo kwa ujasusi wa Urusi ambao utatumia muda tena kuja kuuimarisha.

Kufurushwa kwa wanadiplomasia kumekuja kama majibu ya kile mataifa hayo yanasema Urusi ilihusika katika kutumia sumu dhidi ya jasusi wake wa zamani Sergei Skripal na mtoto wake Yulia.

Awali nchi ya Uingereza iliwafurusha nchini mwake wanadiplomasia zaidi ya 23 baada ya kuilaumu Serikali ya Moscow kwa shambulizi hilo.

Siku ya Jumanne nchi ya Urusi imesema itajibu mapigo hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.