Pata taarifa kuu
HISPANIA-UJERUMANI

Hispania: Puigdemont mahakamani Ujerumani, wafuasi wake waandamana

Rais wa zamani wa Catalonia Carles Puigdemont Jumatatu ya wiki hii atapandishwa kizimbani kwenye mahakama ya nchini Ujerumani baada ya kukamatwa mwishoni mwa juma na polisi ya Ujerumani akivuka mpaka kutoka Denmmark.

Maelfu ya waandamanaji kwenye eneo la Catalonia ambao ni wafuasi wa Puigdemont wakiandamana kupinga kukamatwa kwake nchini Ujerumani. Machi 25, 2018.
Maelfu ya waandamanaji kwenye eneo la Catalonia ambao ni wafuasi wa Puigdemont wakiandamana kupinga kukamatwa kwake nchini Ujerumani. Machi 25, 2018. REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kukamatwa kwake kumeibua maandamano makubwa ya wafuasi wake kwenye mji wa Catalonia, maandamano ambayo polisi walilazimika kutumia nguvu kuwakabili.

Polisi wa Ujerumani walimkamata Puigdemont siku ya Jumapili baada ya kuvuka mpaka akitokea Denmmark ambapo kukamatwa kwake kuliutokana na waranti ya umoja wa Ulaya.

Kukamatwa kwake kumekuja ikiwa ni miezi 5 imepita tangu Puigdemont akimbie nchi yake kukwepa kukamatwa na waendesha mashtaka wa Uhispania waliotaka kumshtaki kwa makosa ya uhaini na uasi kutokana na wito wake wa kutaka eneo la Catalonia kujitenga.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake Jaume Alonso-Cuevillas, amesema Puigdemont alikuwa njiani kuelekea Ubelgiji ambako alikuwa amekimbilia huko tangu atake kutawala eneo la Catalonia kwa nguvu.

Puigdemont atapelekwa mbele ya majaji wa mahakama kuu kuthibitisha uraia wake na mahakama itaamua ikiwa abakie kizuizini kusubiri kusafirishwa kwake au la.

Makabiliano ya polisi na waandamanaji yameshuhudiwa kwenye miji mingi ya Catalonia punde tu baada ya kukamatwa kwake.

Polisi walitumia risasi za mpira na mabomu ya kutoa machozi kukabiliana na waandamanaji ambao nao walikuwa wakirusha chupa za maji na mayai kuwalenga polisi.

Watu 90 wamejeruhiwa wakati wa maandamano hayo mjini Barcelona wakiwemo polisi 22, wamesema madaktari waliowasaidia waandamanaji.

Watu wengine 7 walijeruhiwa kwenye maandamano ya mjini Lleida ulioko umbali wa kilometa 150 magharibi mwa mji wa Barcelona na mtu mwingine mmoja alijeruhiwa kwenye mji wa Tarragona kusini mwa mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.